Enock Maregesi's Blog: Kolonia Santita (Laana Ya Panthera Tigrisi), page 3

March 18, 2018

Mke Tu Mtu Unahama, Ije Iwe Chama?






269. Mke tu mtu unahama, ije iwe chama? Na mke ulichagua mwenyewe, hukuchaguliwa na wananchi.


Vivyo hivyo: mume tu mtu unahama, ije iwe chama? Na mume ulichagua mwenyewe, hukuchaguliwa na wananchi.


Kuhama chama ni haki ya mtu ya msingi kabisa ya kidemokrasia. Lakini kumbuka, kuvunja mkataba lazima ulipe.





Advertisements
1 like ·   •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on March 18, 2018 16:00

March 16, 2018

COSOTA









Nimekamilisha usajili wa Kolonia Santita katika idara mbalimbali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; kama vile BASATA, COSOTA, COSTEC, Maktaba ya Kihistoria ya Makumbusho ya Taifa, Maktaba Kuu ya Taifa, na Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, kwa ajili ya utafiti na vizazi vijavyo.


 


Wasilisha nakala ya kazi yako kwa mujibu wa sheria. Taifa ni mataifa. Ukitambuliwa na taifa utatambulika kimataifa.


 


Kabla hawajakupiga kwa sheria wapige kwa kujisajili.
 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on March 16, 2018 01:14

March 11, 2018

Ukiwa na Maarifa Utaomba Kile Unachostahili Kupata

[image error]



268. Ukiwa na maarifa utaomba kile unachostahili kupata. Lakini ukiwa huna utaamrisha.


Watu hawajui kuomba ndiyo maana Mungu akasema tushukuru kwa kila jambo, jema au baya, kwa sababu tutabarikiwa kulingana na fadhila na rehema zake.


Watu badala ya kumwomba Mungu wanamwamrisha. Mtumwa hawezi kumshauri bwana wake, sembuse mwanadamu kumwamrisha Mungu?


Mungu anasema katika Isaya 45:11, “Bwana, Mtakatifu wa Israeli, na Muumba wake, asema hivi; Niulize habari za mambo yatakayokuja; mambo ya wana wangu, na habari ya kazi ya mikono yangu; haya! Niagizeni.” Lakini je! Hivyo ndivyo Mungu anavyomaanisha? Kwamba tumwamrishe yeye? Mungu anamaanisha tupeleke shida zetu kwake kwa sababu hakuna mungu mwingine isipokuwa yeye. Kama hatajibu, shida zetu hazitajibiwa.


Kwa sababu Isaya 45:9-10 inasema, “Ole wake ashindanaye na Muumba wake! Kigae kimoja katika vigae vya dunia! Je! Udongo umwambie yeye aufinyangaye; Unafanya nini? Au kazi yako, Hana mikono? Ole wake amwambiaye baba yake, Wazaa nini? Au mwanamke, Una utungu wa nini?”


Unaona? Mungu hawezi kuwa mtumwa, nasi hatuwezi kuwa Mungu. Mungu ataendelea kutuamrisha, nasi kupitia Roho wa Mungu tutaendelea kuomba kile Mungu alichopanga tupate.

 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on March 11, 2018 16:00

March 9, 2018

Taabu ya Yakobo

[image error]


Irani itakapoipiga Israeli, kama ambavyo imeshaahidi, Israeli itajibu mapigo. Kwa vile Israeli ina nguvu zaidi kuliko Irani, itaipiga Irani kwa silaha za kawaida. Itaipiga hata kwa silaha za kinyukilia pia.


Kutunisha misuli, Irani itaomba msaada wa kijeshi kutoka katika nchi za Kiarabu; ambazo zitakubali kuingilia kati na kuisaidia Irani. Kwa silaha za kawaida, bado nchi zote za Kiarabu zitakazokubali kuisaidia Irani hazitakuwa na uwezo wa kuishinda Israeli. Kuishinda itabidi zitumie silaha za kinyukilia.


Silaha za kinyukilia zitakapoanza kutumika, Marekani itaingilia kati kuisaidia Israeli. Marekani itakapoingilia kati kuisaidia Israeli, Urusi itaingilia kati kuisaidia Irani. Ufaransa, Uingereza na Ujerumani zitaingilia kati kuisaidia Israeli; huku China ikiingilia kati kuisaidia Irani. Hapo Vita Kuu ya Tatu ya Dunia itaanzishwa rasmi.


Katika vita hiyo ya kinyukilia na mbaya kuliko vita zote zilizowahi kupiganwa, Israeli itashinda vita na itaanzisha utawala wa Mpinga Kristo duniani kote. Kutakuwa na dini moja. Kutakuwa na serikali moja. Kutakuwa na sarafu moja. Watu watapungua hadi kufikia milioni 500, kama ilivyokuwa mwaka 1650, asilimia 7 ya idadi ya watu wote ya leo.


Wafuasi wa Yesu Kristo watapata taabu kubwa ambayo haijawahi kutokea. Yeyote atakayempinga Mpinga Kristo, yeyote atakayepinga utawala wa Mpinga Kristo, atakiona cha mtema kuni. Watu wengi watauwawa kwa sababu ya ufuasi wao kwa Masihi. Wale watakaokuwa na talanta ya kuhubiri watauwawa kinyama, hadharani, ili liwe fundisho kwa wafuasi wengine wa Yesu Kristo.


Miongoni mwa wale watakaokuwa wanahubiri injili ya kweli ya ufalme wa Mungu bila woga wa aina yoyote ile, atakuwemo Eliya na Enock. Eliya na Enock Mungu aliwachukua bila kuonja mauti, kama akiba, kwa sababu ya kipindi hicho cha Taabu ya Yakobo.


Eliya na Enock wataibuka ghafla jijini Yerusalemu na kuanza kuhubiri injili ya kumpinga Mpinga Kristo. Kwa vile hawataogopa chochote, wala hawatamwogopa yeyote, serikali ya Israeli itawakamata na kuwatesa lakini hawatanyamaza.


Mpinga Kristo atakapoona imeshindikana kuwanyamazisha, Eliya na Enock, huku akitamba kwamba yeye ndiye Yesu Kristo ambaye kila mtu ndiye aliyekuwa akimsubiri arudi kwa mara ya pili; na kwamba yeye anatoka katika ukoo wa mfalme Daudi, ili watu waamini kama kweli yeye ndiye Yesu Kristo, ataamuru Eliya na Enock wauwawe hadharani kama wahubiri wengine.


Eliya na Enock watakapouwawa, Mungu atawafufua na watarudi mbinguni wakiwa wameonja mauti kama binadamu mwingine yeyote yule. Hapo mlango wa rehema utakuwa umefungwa. Muda wowote kuanzia hapo Yesu atarudi, kwa mara ya pili, na kwa ajili ya ufufuo wa kwanza.


Watakatifu wote watanyanyuliwa na wataondoka pamoja na Yesu kuelekea mbinguni, kwa ajili ya ziara ya miaka 1000 katika ulimwengu wa roho; kuanzia dunia ya kwanza ya ulimwengu huo iitwayo Asiyah hadi ya mwisho iitwayo Adam Kadmon, katika mji mpya wa Yerusalemu.


Baada ya milenia, kipindi hicho huku duniani Ibilisi akiwa kifungoni na malaika wake, binadamu wote wenye dhambi wakiwa wamekufa, Yesu na watakatifu wote atarudi kwa ajili ya ufufuo wa pili; na kama mfalme wa ulimwengu wote milele.


Wenye dhambi watafufuliwa na wataungana na Ibilisi kuipiga Yerusalemu Mpya itakayokuwa inang’inia hewani, huku Yesu na watakatifu wote wakiwa hawana silaha yoyote; lakini vilevile wakiwa hawapigwi kwa silaha yoyote.


Shetani atakapoonekana kushindwa, Yesu atawasha ‘kibiriti cha kiroho’. Mafuta yote yaliyopo ardhini dunia nzima yatalipuka na kugeuza ardhi yote kuwa ziwa la moto, na hivyo wenye dhambi wote kupata aibu ya milele.


Katika Biblia kuna tabiri 333 kuhusu maisha ya Yesu Kristo, na kuhusu kurudi kwake kwa mara ya pili. Kati ya hizo, 332 zilitimia! Bado mmoja tu: Kurudi kwa Yesu Kristo kwa mara ya pili.


Unadhani huo wa kurudi kwa Yesu Kristo kwa mara ya pili hautatimia? Muda umefika. Jitathmini katika maisha yako na uchague lililo jema.

 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on March 09, 2018 04:59

March 4, 2018

Hakuna Magonjwa

[image error]




267. Hakuna magonjwa. Magonjwa yote yamo akilini mwetu. Ukitaka kulithibitisha hilo nenda hospitali yoyote ya Dar kisha toa tangazo la sauti kwamba Al-Shabaab wako nje watalipua jengo zima kwa mabomu. Asilimia 95 ya hao unaosema ni wagonjwa watakimbia hadi Bagamoyo.


 


Uongo wa daktari ni ukweli wa mgonjwa. Wakati mwingine maneno mazuri na huduma nzuri humponyesha mgonjwa. Kataa magonjwa yote kwa damu na jina la Yesu.


 


Tunaona magonjwa nje, nje ya akili zetu, ili tuone ni wapi tumekosea, ili tujirekebishe kwa ndani.


 


Magonjwa yote tunayoyaona watu wakiugua au sisi wenyewe tukiugua yako ndani ya akili zetu. Tunayaona nje, ya akili zetu, ili tuwe na uhusiano na magonjwa hayo, kusudi tuone ni wapi tumekosea, ili tujirekebishe kwa ndani. Kwa hiyo kama mtu anaumwa malaria ujue ndani ya akili yako kwamba malaria ni ugonjwa mbaya, na ujirekebishe kwa maana ya kujikinga na mbu wanaosababisha malaria. Hiyo ndiyo asili yetu. Hivyo ndivyo Mungu alivyotuumba na alituumba hivyo kwa manufaa yetu.


 


Ukiona mtu anaumwa au wewe mwenyewe unaumwa ujue ni ujumbe kutoka ndani unaokusihi ubadilike, uwe kama Mungu anavyotaka uwe.
 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on March 04, 2018 15:00

February 25, 2018

Kula, Lazima Tuue!

[image error]


266. Maisha ni muuaji na yanatulazimisha kuishi. Kula, lazima tuue!


Kama maisha ni muuaji na yanatulazimisha kuishi, uhuru wa kuchagua tutautoa wapi? Mathalani, bila chakula au hewa tutaishi vipi? Tuna uhuru wa kuchagua mema au mabaya, lakini hatuna uhuru wa kuchagua mambo mengine. Hatuna jinsi. Lazima tule. Lazima tuvute hewa.


Kila tunapokula na kunawiri kama binadamu tunakula kitu ambacho hapo awali kilikuwa kikiishi, lakini sasa kimekufa. Kondoo analiwa akiwa hai, au akiwa amekufa, lakini hicho kipande kinacholiwa akiwa hai au amekufa seli zake zimekufa. Tunalazimishwa kula vitu ambavyo tayari vimeshakufa.


Kwa mfano, kuna watu hawapendi kula. Wanalazimisha tu. Lakini hawana jinsi. Lazima wale ili waishi. Hata hivyo, hali hiyo hubadilika unapoingia Asiyah. Asiyah ni sayari ya kwanza ya ulimwengu wa roho. Sayari nyingine za ulimwengu wa roho ni Yetzirah, Beriah, Atzilut na Adam Kadmon. Adam Kadmon ndipo anaposemekana kuishi Mungu.


Sayari zote hizo zimetajwa kimafumbo katika kitabu cha Isaya 43:7: “Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya.”


Atzilut maana yake ni ukaribu (‘jina langu na utukufu wangu’). Beriah maana yake ni uumbaji (‘niliyemwumba’). Yetzirah maana yake ni ufanyaji wa jambo (‘nimemfanya’). Asiyah maana yake ni tendo la kufanya jambo.


Ulimwengu wa roho hujulikana pia kama ABiYA, ambacho ni kifupi cha majina ya sayari zake tano.


Kwa nini tulizaliwa bila kuomba? Kwa nini wakati tunazaliwa hatukuwa na uhuru wa kuchagua tuzaliwe wapi au tuzaliwe kwa wazazi gani? Watu wengi wangependa kuzaliwa katika nchi nzuri au kwa wazazi wenye pesa. Lakini hivyo sivyo ilivyokuwa na haitaweza kuwa hivyo. Kwani asili yetu ni sehemu ya usawa wa ulimwengu huu na usawa wa asili ya maisha yetu.


Sisi ni watumwa; hatuna uhuru; na kwa bahati mbaya tutaendelea kuwa hivyo hadi mwisho wa dunia, kwa sababu hatuna uwezo wa kubadili asili yetu ya kibinadamu tukiwa ulimwenguni. Tunao uwezo wa kufanya hivyo tukiwa katika ulimwengu wa roho.


Hivyo, kuwa huru, kuwa raia wa ulimwengu wa roho. Ukitaka kuwa raia wa ulimwengu wa roho, kuwa rafiki (wa kweli) wa Neno la Mungu.

 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on February 25, 2018 15:00

February 18, 2018

Elimu ni Ufunguo wa Maisha

[image error]



265. Elimu ni ufunguo wa maisha. Lakini wengine funguo zao zina kutu.


Funguo zikiwa na kutu hazitafungua vizuri makufuri. Wenye funguo zenye kutu ni wababaishaji wa maisha, nami nikiwemo.

 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on February 18, 2018 15:00

February 11, 2018

Shida na Raha

[image error]


264. Tunaumbwa kwa mfano wa Mungu kupitia shida na raha, kwa sababu ya ukaidi wa asili yetu kama binadamu. Bila shida na raha hatutakomaa wala hatutakamilika. Wakati mwingine Mungu anatufinya ili tusikie.


Ukaidi ni asili ya binadamu. Si rahisi kuibadili, hadi ujue wewe ni nani na kwa nini ulizaliwa. Ukijua wewe ni nani na kwa nini ulizaliwa utaishi sawasawa na mapenzi ya Mungu kwa binadamu.


Wenye shida katika Bwana wamebarikiwa. Wenye furaha ni wale wasiokuwa na furaha.


Kidunia wenye furaha ndiyo tunaosema wamebarikiwa. Lakini Kimungu wenye furaha ni wale wasiokuwa na furaha kwa sasa, lakini wenye hakika ya kuwa na furaha kwa baadaye. Yaani, kidunia wenye shida katika Bwana ndiyo tunaosema wamebarikiwa. Fungua moyo wako, ili uwe mkunjufu na mnyenyekevu.


Chochote kinachotokea katika maisha yako Mungu anakupa njia ya kufika pale anapotaka ufike. Jifunze lugha ya maisha ambayo Mungu anajaribu kuongea na wewe.

 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on February 11, 2018 15:00

February 5, 2018

Woga Wako Umaskini Wako

[image error]


263. Mbele ya simba simama kidete usitetemeke miguu. Kisha mwangalie machoni bila woga wa aina yoyote ile, hata akikutisha vipi.


Mfalme Nebukadneza alipouvamia mji wa Yerusalemu na kuushinda katika mwaka wa tatu wa utawala wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, aliagiza baadhi ya wana wa Israeli aondoke nao kurudi Babeli, kati ya mwaka 605 na 562 Kabla ya Kristo. Vijana watatu: Hanania, Mishaeli na Azaria (pamoja na Danieli) walichukuliwa katika kundi la kwanza la mateka.


Walipofika Babeli, maili 25 kusini kwa Baghdad ya leo, vijana hao walipewa majina mapya. Hanania aliitwa Shadraki, Mishaeli aliitwa Meshaki, na Azaria aliitwa Abednego.


Shadraki, Meshaki na Abednego mara tu baada ya kufika Babeli walijaribiwa kulingana na imani yao. Lakini walisimama kidete kumtetea Mungu wao, hata mfalme alivyowatisha vipi. Kwa sababu hiyo, Mungu aliwapa maarifa na uelewa wa kila aina ya fasihi na elimu ya Mesopotamia.


Walipoulizwa maswali na mfalme na watu wenye hekima, Shadraki, Meshaki na Abednego walionekana kuwa na akili mara kumi zaidi ya mtu mwingine yeyote yule katika Ufalme wa Babeli. Kwa hiyo, mfalme akapendezwa nao. Akawatunuku vyeo mbalimbali katika jumba la kifalme.


Baadaye mfalme Nebukadneza aliota ndoto ambayo hakuikumbuka. Watu wenye hekima na wachawi wa Babeli waliposhindwa kumfunulia ndoto yake, mfalme aliamuru wauwawe wote lakini wakaokolewa na Danieli. Danieli alimfunulia mfalme ndoto yake, akaitafsiri kabisa, hadi mfalme akaridhika na kufurahishwa naye.


Kutokana na ndoto hiyo mfalme Nebukadneza aliamua kutengeneza sanamu la dhahabu kama mungu wa kuabudiwa. Sanamu hilo lililokuwa na urefu wa futi tisini na upana wa futi tisini na la dhahabu tupu, kwani inasemekana huko Babeli dhahabu ilikuwa nyingi kuliko vumbi, lilikuwa utabiri wa mwanzo wa Ufalme wa Nebukadneza na mwisho wa Ufalme wa Rumi, ambapo hakuna taifa lolote kubwa katika dunia ya leo litaungana na taifa dogo hadi mwisho na mwanzo wa dunia mpya.


Kisha mfalme akatuma watu kukusanya maamiri, manaibu, maliwali, makadhi, watunza hazina, mawaziri, mawakili, na wakuu wa wilaya zote, ili wahudhurie wakati wa kumzindua mungu huyo, mfalme Nebukadneza aliyemtengeneza.


Kutokana na umuhimu wa sanamu mfalme Nebukadneza aliwatahadhalisha watu hao yatapa 100; kuwa yeyote yule ambaye hangesujudu na kumwabudu mungu wa dhahabu, pindi sauti ya panda na filimbi na kinubi na zeze na santuri na zomari na namna zote za ngoma itakaposikika, atatupwa saa hiyohiyo katika tanuru la moto uwakao.


Lakini sauti ya vyombo hivyo iliposikika, Shadraki, Meshaki na Abednego hawakutii amri ya mfalme hata kidogo. Mfalme alipopewa taarifa kwamba Shadraki, Meshaki na Abednego hawakutii amri yake alikasirika sana. Lakini alipowapa nafasi nyingine ili wasujudu na kuabudu, bado Shadraki, Meshaki na Abednego hawakufanya kama mfalme alivyotaka wafanye.


Kitendo hicho hakikuwa kizuri! Mfalme bila kuchelewa alitoa amri ili Shadraki, Meshaki na Abednego watupwe haraka katika tanuru la moto. Saa hiyohiyo walikamatwa na kutupwa katika tanuru, la moto uliowaka mara saba zaidi, kama mfalme alivyoagiza.


Lakini cha kushangaza, Shadraki, Meshaki na Abednego hawakuwa peke yao, na hawakuunguzwa hata kidogo na moto wa tanuru, hadi mfalme akaogopa na kuwaita watoke nje.


Nebukadneza alipogundua kuwa hawakuwa na jeraha lolote la moto, wala hawakunuka moshi wala hawakuwa na dalili yoyote ya kuwa tanuruni, toka siku hiyo akamwamini Mungu wa Shadraki, Meshaki na Abednego; na akaamuru ufalme mzima wa Babeli kufanya hivyo. Masanamu zaidi ya 200 yaliyokuwa yakiabudiwa kama miungu yakateketezwa. Huo ndiyo ukawa mwanzo wa Mesopotamia kumwamini Yehova.


Baada ya hapo mfalme aliwapandisha vyeo Shadraki, Meshaki na Abednego katika nyadhifa mbalimbali za kifalme! Walifanikiwa. Ujasiri wao ulifanya wawe matajiri wa mbinguni na duniani.


Katika dunia ya leo mfalme Nebukadneza ni simba; na simba ni Shetani. Shadraki, Meshaki na Abednego ni mimi na wewe. Tanuru la moto uwakao ni shida inayokukabili katika maisha yako.


Tatizo lako hata liwe kubwa kiasi gani, si lako kulipigania. Mwachie Mungu. Kila mtu ana simba wake katika maisha yake, na ana tanuru lake katika maisha yake; lakini hata simba wako awe mkali kivipi, hata tanuru lako likichochewa moto kiasi gani, usitetemeke miguu wala usiogope chochote.


Kama wana wa Israeli waliweza kusimama kidete mbele ya simba na ndani ya tanuru, katika kipindi ambacho watu hawakumjua Mungu nje ya Israeli, mimi na wewe tutashindwa vipi leo?


Kuwa jasiri mbele ya simba na tanuru la maisha yako, kusudi mwisho wa siku Mungu atakapokutofautisha kimaisha, uende zako paradiso. Ukiogopa kushindwa hutashinda. Woga wako ndiyo umaskini wako.

 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on February 05, 2018 02:00

January 29, 2018

Serikali Haitambui Wahuni




Wakati unaokubalika ni sasa. Ukijitambulisha utatambulika, usipojitambulisha hutatambulika. Serikali haitambui wahuni.

 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on January 29, 2018 02:29

Kolonia Santita (Laana Ya Panthera Tigrisi)

Enock Maregesi
Riwaya ya Kiswahili ya kijasusi kutoka kwa Enock Maregesi.
Follow Enock Maregesi's blog with rss.