Enock Maregesi's Blog: Kolonia Santita (Laana Ya Panthera Tigrisi), page 4

January 28, 2018

Kwa Pamoja Tuijenge Nchi Yetu

[image error]




Usipojisajili BASATA watasema una kiburi. Serikali hupenda watu iliyoridhika nao. Wasanii wote nendeni BASATA mkajisajili.


 


BASATA (Baraza la Sanaa la Taifa) hawataweza kukutambua kwa sababu hujajisajili kwao, na kushirikiana na msanii ambaye hajajisajili BASATA ni kinyume cha sheria.


 


Kupeperusha bendera ya taifa kwa niaba ya taifa bila kujisajili serikalini ni kosa la jinai, na serikali haitakutambua kwa sababu wewe mwenyewe hujajitambua.


 


Mambo madogomadogo yanayohusu serikali si ya kudharau. Kama unavyoona umuhimu kukata leseni ya gari lako, ona umuhimu hivyohivyo kujisajili serikalini.


 


Unataka kuondoa dhambi lakini hukutani na wenye dhambi. Hiyo dhambi utaiondoaje?


 


Kazi yenu kwetu ni kutusaidia, na kazi yetu kwenu ni kuwasaidia pia; kwani kila mwananchi anao wajibu wa kuisaidia serikali yake. BASATA, katika jina la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, endeleeni kuhamasisha na kuhakikisha wasanii wote nchini wanajisajili; kwa kuendelea kutoa tuzo mbalimbali za sanaa na jitihada nyingine, na kwa kuendelea kufuatilia kuhakikisha kuwa kila msanii anajisajili na kupata kibali.


 


TRA wanahamasisha na kufuatilia watu walipe kodi. BASATA hamasisheni na kufuatilia wasanii wajisajili.


 


Kujisajili ni lazima kwa mujibu wa sheria, lakini si kila msanii ambaye hajajisajili BASATA anajua kuwa anafanya kosa.


 


Kwa pamoja tuijenge nchi yetu.
 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on January 28, 2018 22:44

Hakuna Ufalme Unaokuja Mara Mbili

[image error]




262. Linda mafanikio yako. Hakuna ufalme unaokuja mara mbili.


 


Kila ufalme una enzi yake. Ukishapita umepita. Hata kama utarudi hautakuwa sawa na wa kwanza.


 


Linda mafanikio yako kwa kulinda akili yako, lakini kwa upendo na wema kwa wenzako. Huwezi kufanya tendo leo likafanana kesho. Kila tendo ni la kipekee, ni la aina yake. Vivyo hivyo, kila ufalme ni wa kipekee na ni wa aina yake.


 


Mafanikio si lelemama. Kuyapata ni shida. Kuyalinda ni shida. Linda mafanikio yako kuacha heshima-kumbukizi. Heshima-kumbukizi ni enzi, heshima, itakayokumbukwa baadaye.
 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on January 28, 2018 15:00

January 26, 2018

Huwezi Kutawala Dunia Bila Elimu

[image error]


Shetani lengo lake ni kutawala dunia. Huwezi kutawala dunia bila elimu!


Shetani anajua kwamba sisi ni warithi wa wokovu na kwamba dunia hii ni kitu kilichoahidiwa kwa Ibrahimu na watoto wake. Sisi wote ni watoto wa Ibrahimu. Anajua kabisa kwamba baadaye sisi ndiyo tutakaokuwa watawala halisi wa dunia hii. Hivyo, anajitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wote ili hilo lisitokee. Shetani na malaika wake ni wengi sana, na wanatumia kila silaha waliyokuwa nayo kutawala dunia.


Inavyoonekana, kadiri mtu anavyozidi kupata elimu ndivyo anavyozidi kudharau uwepo wa Shetani na uwepo wa Mungu pia. Lakini, kwa upande mwingine, ndivyo anavyoonekana hajasoma sana na ndivyo Shetani anavyozidi kulaumiwa kwa kila dhambi inayotendeka. Kuna elimu ya kidunia na kuna elimu ya kidini. Huwezi kutawala dunia bila elimu ya kidunia, kwa sababu Shetani anajua ukiipata elimu hiyo hutajua kama yupo; na huwezi kutawala dunia bila elimu ya kidini, kwa sababu Mungu anajua ukiipata elimu hiyo utajua kama yupo. Hivyo, utamdharau Mungu ukipata elimu ya kidunia, utamheshimu Mungu ukipata elimu ya kidini.



Kama Shetani anatumia elimu kutawala dunia kama vile Mungu anavyotumia elimu kutawala dunia, nani alisema kuwa baadhi ya wasanii wa ‘Bongo Movie’ na ‘Bongo Flava’ ni wanachama wa chama cha siri cha kusaidiana cha wajenzi huru? Je, wana elimu? Jibu unalo.


Anayesema fulani ni mwanachama wa chama cha siri cha kusaidiana cha wajenzi huru ana hakika? Haya mambo ni siri. Amejuaje? Kumbuka, usiamini, jua.


Kama wana elimu wanaweza kuwa wajenzi huru; lakini kama hawana elimu, hawawezi kuwa wajenzi huru.


Shetani ni mjanja sana. Anajua bila elimu hataweza kutawala dunia, baada ya mpango wa Mungu kukamilika. Anajua, mtu akipata elimu ni rahisi sana kujua kama Shetani hayupo. Hivyo Shetani atatimiza malengo yake bila watu kujua.


Mungu hatakubali kuwa na mtu katika ufalme wake ambaye hatakubali kutawaliwa naye. Usikubali kutawaliwa na Ibilisi, kubali kutawaliwa na Mungu. Ni jukumu letu kuanza kuishi sasa kama vile tutakavyoishi mbinguni. Shetani anataka uwe na hekima ya duniani ili akupumbaze. Lakini hofu ya Mungu ndiyo msingi wa hekima ya kweli. Ukitaka asikupumbaze, pokea roho ya Mungu kwa kubatizwa. Ukiipokea roho ya Mungu utajua mambo ya Mungu, ambayo dunia haiwezi kujua.


Usipoangalia kwa undani sana, Shetani anatutawala kwa sababu hatuna uwezo wa kumwona. Aidha, bila hata sisi kujua, anaweza kuwasiliana nasi kimawazo na kitabia kupitia hewa hiihii inayotusaidia katika kuishi.


Wengi katika dunia hii hawajui kama wanadanganywa au walishadanganywa tayari. Shetani hataki tujue kama anatudanganya au ameshatudanganya tayari, na hataki tujue kama yuko hapa kwa ajili ya kutudanganya sisi. Tunajua tu kwa sababu Neno la Mungu hudhihirisha ukweli huu kupitia Roho Mtakatifu na malaika wema, na tunauamini.


Licha ya hili jambo kutokea katika maisha yetu, Shetani bado anaweza kutudanganya hadi pale tutakapoerevuka kwa kiasi cha kutosha kuhakikisha kwamba udanganyifu huo hautatokea tena.

 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on January 26, 2018 05:49

January 21, 2018

Tengeneza Akili

[image error]


261. Gari lako likiharibika kisha ukashindwa kulitengeneza si gari. Akili yako ndiyo imeharibika. Tengeneza akili yako.


Kwa nini hatuna hela au muda? Akili zetu zimeharibika. Tengeneza akili yako kutengeneza maisha yako.


Vuka mpaka wa ulimwengu wa nyama na ulimwengu wa roho kupata akili ya kuishi mbinguni ulimwenguni.


 

 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on January 21, 2018 15:00

January 14, 2018

Watu Wenye Upara Wanajidai Sana

[image error]



260. Watu wenye upara wanajidai sana. Wanasema kuwa wana sehemu ndogo sana ya kuchana nywele. Lakini hawajui kuwa wana sehemu kubwa sana ya kunawa uso.


Ulichopewa wewe mwenzako amenyimwa na mwenzako alichopewa wewe umenyimwa. Tafadhali, tuheshimiane!

 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on January 14, 2018 15:00

January 11, 2018

Mjinga au Mpumbavu

[image error]


Mtu akikuita mjinga au mpumbavu juu ya maisha yako usikasirike kwa sababu wewe si mjinga wala mpumbavu. Sema hapana kwa ndiyo nyingi kwa sababu hawapaswi kuingilia mambo ya mtu mwingine bila idhini ya Mwenyezi Mungu. Kuingilia mambo ya mtu mwingine bila idhini ya Mwenyezi Mungu ni dhambi, tena dhambi kubwa, ni kuvunja amri kuu ya kwanza ya Mungu.


Mungu ana mpango na maisha ya kila mtu hapa duniani bila kujali dini, jinsia, kabila, rangi, taifa, au umri, na kila mtu ni wa kipekee.



Usiingilie mambo ya mtu mwingine bila kibali kutoka kwa Mungu. Kuingilia mambo ya mtu mwingine bila kibali kutoka kwa Mungu ni dhambi. Dhambi hiyo itakuathiri. Hivyo, jali mambo yako – ya mwingine Mungu anayafanyia kazi – hadi utakapoitwa na Mungu kuingilia kati. Kuingilia kati mambo ya mtu mwingine kunaweza kuathiri mpango wa Mungu katika maisha yake. Hivyo, acha.


Kama John Doe ana matatizo katika maisha yake acha ayatatue mwenyewe. Akishindwa atakuomba ushauri au ataomba ushauri kutoka kanisani kama ni Mkristo, au msikitini kama Mwislamu, au kutoka katika nyumba yoyote ya ibada kulingana na imani yake. Mtu akikuomba ushauri mshauri kwa moyo wako wote, wala usimshauri kwa unafiki au kinyongo cha aina yoyote ile.


Wewe kuingilia mambo ya John ni sawa na kusema, “Mungu umeshindwa hebu ngoja na mimi nijaribu; ngoja niingilie kati kukusaidia juu ya maisha ya John Doe.” Hiyo ni dhambi. Tena ni dhambi kubwa. Unajifananisha na Mungu; kwamba Mungu wa John Doe ameshindwa kwa hiyo mungu wewe ndiye utakayemtatulia matatizo yake.


Amri kuu ya kwanza ya Mungu inasema, “Usiwe na miungu mingine ila mimi.” Kuingilia mambo ya John tayari umevunja amri ya kwanza ya Mungu kwa kujifanya Mungu. Mungu ana mpango na maisha ya John, na anatumia matatizo yake kumfikisha kwenye takdiri aliyompangia. Hivyo, wewe si Mungu, acha Mungu afanye kazi yake. Mungu akikuruhusu kuingilia kati, yaani John akiamua kwa hiari yake mwenyewe kukuomba msaada wa mawazo au ushauri, maana yake ni kwamba Mungu amekuchagua wewe kuwa sehemu ya mafanikio ya John Doe.


“Historia ya maisha yangu ni yangu. Wewe ni nani kusema historia yangu si ya kweli?” –Enock Maregesi


Umesikia mtaani kwamba mke wa kaka yako anatembea na teja, na ukathibitisha, lakini bila kaka yako au shemeji yako kujua. Je, utamwambia kaka yako? Je, utamwambia shemeji yako? Je, utawambia watu wengine? Jibu unalo.

 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on January 11, 2018 05:13

January 8, 2018

Usalama wa Taifa ni Akili si Ukali

[image error]



Usalama wa Taifa ni akili si ukali. Kazi yake, au wajibu wake; ni kukusanya, kuchanganua, kudurusu na kuunganisha kwa makini, taarifa nyeti za kijasusi za ndani na nje ya nchi kuilinda Tanzania na watu wake. Ukitaka kuwa na akili kuwa kawaida. Ukitaka kuwa na nguvu kuwa mkarimu. Ukitaka kuwa tajiri kuwa tajiri wa unyenyekevu.


Kama una akili kuwa kawaida. Kama una nguvu kuwa mkarimu. Kama una pesa kuwa mnyenyekevu. Ukitaka kuwa na akili kuwa kawaida. Ukitaka kuwa na nguvu kuwa mkarimu. Ukitaka kuwa na pesa kuwa mnyenyekevu.

 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on January 08, 2018 12:05

January 7, 2018

SERIKALI HAINA ROHO!

[image error]



259. Serikali haitumii moyo kufanya maamuzi yake. Inatumia akili.


“Serikali haina roho!” –Enock Maregesi


Ukiona serikali inafanya jambo la ajabu, kama vile kubomoa nyumba za watu na za kwake yenyewe, huku watu wakilalamika lakini yenyewe hailalamiki, ujue haitumii moyo, inatumia akili. Inafanya hivyo kwa faida ya baadaye ya nchi.

 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on January 07, 2018 15:00

January 2, 2018

Nenda Bethlehemu

[image error]


Bethlehemu iliteuliwa na Mungu kuwa mahali pa kuzaliwa Mfalme. Kwa sababu ya Bethlehemu, dhambi zetu zote zilisamehewa. Wakristo wengi wakipata pesa wanakwenda Dubai, China, Marekani, Uingereza, na mahali pengine kutalii. Lakini hawaendi Bethlehemu.


 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on January 02, 2018 22:15

December 31, 2017

Mwaka Mpya 2018

[image error]


258. Mwaka 2018 ni mwaka wa kujitambua. Andika maisha yako kwenye nukuu.


Nukuu ni nahau yenye mantiki na maadili ya busara iliyojificha. Nahau inaweza isiwe na mantiki, lakini ni fungu la maneno liletalo maana.


Tafuta nukuu itakayokuongoza katika maisha yako, na usiwe wa Shetani, mwaka mzima.


Kila mtu anapaswa kuwa na nukuu yake mwenyewe katika maisha yake.



 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on December 31, 2017 15:00

Kolonia Santita (Laana Ya Panthera Tigrisi)

Enock Maregesi
Riwaya ya Kiswahili ya kijasusi kutoka kwa Enock Maregesi.
Follow Enock Maregesi's blog with rss.