Enock Maregesi's Blog: Kolonia Santita (Laana Ya Panthera Tigrisi), page 5

December 30, 2017

Mwaka Mpya

[image error]


Mwaka mpya ukifika watu husherehekea kwa vifijo na nderemo! Pumzi ikifika hawasherehekei. Kwa nini?


Kitu cha kwanza kufanyika mwanadamu anapozaliwa ni kuvuta pumzi ya kwanza katika mapafu ya mwili wake. Cha mwisho kufanyika kabla ya kufa ni kutoa pumzi ya mwisho katika mapafu ya mwili wake. Pumzi iliyoingia kwanza baada ya kuzaliwa, itakuwa ya mwisho kutoka kabla ya kufa.


Pumzi ni bora kuliko muda halafu pumzi ni uhai. Bila uhai watu hawataweza kusherehekea mwaka mpya au kufanya chochote. Likumbuke jina la Mwenyezi Mungu katika kila pumzi unayoingiza na kutoa.


Kwa nini watu wana kawaida ya kuona thamani ya mtu baada ya mtu kufariki? Kwa nini watu wana kawaida ya kuona thamani ya pumzi katika kipindi ambacho mtu hana uwezo tena wa kuvuta hewa? Nini thamani ya pumzi? Thamani ya pumzi ni kukufanya uwe wewe na si udongo.


Biblia inatuambia kuwa tuombe bila kukoma. Lakini tutaombaje bila kukoma? Njia mojawapo ya kufanya hivyo ni kutumia ‘maombi ya pumzi’ kila siku kama ambavyo Wakristo wengi wamekuwa wakifanya kwa karne nyingi.


Unachagua sentensi fupi au maneno rahisi kuhusu Yesu unayoweza kuyasema na kuyarudia kimoyomoyo kila siku katika kila pumzi inayoingia na kutoka ndani ya mapafu yako! Kwa mfano: “Asante Yesu.” “U pamoja nami.” “Nataka kukujua.” “Napokea neema yako.” “Nakutegemea wewe.” “Mimi ni wako.” “Nisaidie nikuamini.” “U Mungu wangu.” “Naishi kwa ajili yako.” “Nisamehe dhambi zangu zote.”


Fundisha akili yako kumkumbuka Mungu kila wakati.



 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on December 30, 2017 22:55

December 24, 2017

Ndani na Nje ya Ufahamu Wako

[image error]




257. Jambo linalofanyika ndani ya ufahamu wako ni lako, lakini lile linalofanyika nje ya ufahamu wako ni la Mungu.


 


Ukiomba jambo kwa Mungu ukiwa na imani uhitaji kuomba tena. Mungu amekusikia. Jibu lako litafika kama mwizi! Kama Yesu atavyorudi kwa mara ya pili, bila mtu yeyote kujua, ndivyo baraka yako itakavyofika.


 


Mathalani unaweza kuwa umetuma barua ya maombi ya kazi hadi ukasahau kama waliipata! Kama hiyo kazi ni yako, siku utakapopata barua ya kuitwa kwa ajili ya mahojiano utakuwa umejisahau! Ukienda kwenye mahojiano utakuwa na nafasi kubwa mno ya kupata hiyo kazi! Lakini ukikumbuka kwamba ulituma barua ya maombi huku ukifungua akaunti yako ya baruapepe, ukitegemea kukuta barua ya kuitwa kwa ajili ya mahojiano na kweli ukaikuta, nafasi ya kupata hiyo kazi ni ndogo mno!


 


Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo; Bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza jambo (Mithali 25:2). Mungu hupenda kufanya mambo yake kwa siri.


 


Ukiomba kitu kwa Mungu mwachie Mungu akusaidie yeye mwenyewe kukifikiria! Ukitaka Mungu akukumbuke, jisahau! Hutajua baraka yako itafika lini!


 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on December 24, 2017 15:00

December 17, 2017

Mungu Ndiye Hakimu Peke Yake

[image error]


256. Mungu pekee ndiye anayeweza kuwa hakimu wa mtu, kwa vile yeye pekee ndiye anayeweza kuwa hakimu wa moyo wa mtu.


Kila mtu anaishi kulingana na hali yake ambayo ni ya kipekee. Tunafanya kazi kwa malengo tofauti, huku tukikua kwa viwango mbalimbali juu ya tabia nyingi tofauti. Tunapata majaribu makubwa yasiyofanana, na tumeathiriwa na mazingira yetu kwa njia nyingi tofauti. Hivyo, kila mtu ni wa kipekee.


Ulinganisho wa kweli na sahihi hauwezekani kwa kujilinganisha na mtu mwingine yeyote yule, kwamba kwa vile mwenzako amefanya kosa basi amekosea. Kosa alilolifanya limo ndani ya mpango wa Mungu. Wewe kusema amekosea umekosoa mpango wa Mungu. Haitawezekana kupata kipimo sahihi cha ukamilifu wa mtu, kati yako na mtu mwingine, kulingana na ukweli wa Mungu.


Mungu pekee ndiye anayeweza kumhukumu mtu kisawasawa, kwa vile yeye anaweza kuhukumu moyo na kuona picha kamili ya maisha ya mtu.



 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on December 17, 2017 15:00

December 13, 2017

Pigana na Mwindaji wa Roho Hadi Roho Yako Ikombolewe

[image error]


Shetani hawezi kujua unafikiria nini: 1 Wafalme 8:39. Yesu anajua unafikiria nini: Yohana 2:25. Shetani haweza kufanya jambo bila ruhusa ya Mungu: Mathayo 4:1. Shetani hawezi kukulazimisha kutenda dhambi: Yakobo 4:7. Pigana na mwindaji wa roho hadi roho yako ikombolewe.


 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on December 13, 2017 04:32

December 12, 2017

Dodge Ram

[image error]


Dodge Ram, gari la majambazi wa Kolonia Santita, lililohusika katika utekaji nyara wa mpelelezi mashuhuri wa Tume ya Dunia kutoka Israeli Daniel Yehuda, lililokuwa na watu saba ndani, liliisindikiza teksi iliyombeba Yehuda; toka Uwanja wa Ndege wa Copenhagen, hadi Msitu wa Mfalme wa Kangelunden, karibu na Ukumbi wa Kimataifa wa Bella Center, huko Tårnby, jijini Copenhagen.


 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on December 12, 2017 14:46

December 10, 2017

Kufanikiwa kwa Nguvu za Nuru Kupitia Nguvu za Giza

[image error]



255. Ukiwa maasumu (ukiwa mwema) hutakuwa na maarifa ya ulimwengu huu na unataka kufanikiwa. Wale waliofanikiwa kutokana na maarifa ya ulimwengu huu hawatakupenda.


Matajiri wengi wamefanikiwa kutokana na nguvu za giza. Ukitaka kufanikiwa kama wao na wewe hupendi nguvu za giza watakuchukia; watakuona huna akili. Kuwasaidia lazima wawe kama wewe; na kukusaidia lazima uwe kama wao.


Wao wamefanikiwa kwa nguvu za giza lakini wewe unataka kufanikiwa kwa nguvu za nuru kupitia nguvu za giza. Unadhani watakusaidia?


Wasaidie, kwa hekima. Bila hivyo, wewe na wao, hamtauona ufalme wa Mungu.


Unaambiwa uende kwa mganga wa kienyeji ili upate hela hutaki. Lakini unaomba hela kwa mtu aliyekwenda kwa mganga wa kienyeji na akapata hela. Ukishirikiana na mwizi, wewe pia ni mwizi.




 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on December 10, 2017 15:00

December 9, 2017

Kwa Nini Biblia Imejaa Mafumbo?

[image error]


Kwa nini Biblia imejaa mafumbo? Biblia imejaa mafumbo kwa sababu akili za watu bado hazijakomaa kuupokea ukweli. Yesu na waandishi wote wa Biblia waliongea na kuandika kimafumbo, ili Neno la Mungu lijidhihirishe lenyewe kiroho katika mawazo ya mtu.


 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on December 09, 2017 00:05

December 8, 2017

Shetani na Uumbaji

[image error]



Lengo kuu la Shetani kuingilia uumbaji wa Mungu kwa kutumia Succubus na Incubus ni kumzuia Yesu asirudi kwa mara ya pili. Anajua akiingilia uumbaji huo na kuwafanya watu wote wawe na roho za kishetani, wokovu hautakuwa na maana, Yesu hatakuwa na mtu wa kumwokoa atakaporudi kwa mara ya pili.


 


Yesu alikuwa binadamu ili afe kama binadamu kwa ajili ya binadamu. Alikufa msalabani ili sisi wote tuokoke. Lakini Shetani hataki hilo litokee. Akiingilia uumbaji wa Mungu toka tumboni mwa binadamu, binadamu atakayezaliwa hatakuwa na uwezo wa kuongoka. Atakuwa na roho ya jini itakayomjua Shetani badala ya kumjua Mungu. Hivyo kurudi kwa Yesu kwa mara ya pili hakutakuwa na maana, kwa sababu hakutakuwepo na mtu wa kuokolewa.


 


Hata hivyo, toka mwaka 1995 watu wengi walianza kuamka kiroho dunia nzima; na mwaka 2012 waliamka zaidi, pale ulimwengu ulipoanza kuhama kutoka kwenye masafa ya ngazi ya nne ya ufahamu wa binadamu (‘4th dimension’) kwenda kwenye masafa ya ngazi ya tano ya ufahamu wa binadamu (‘5th dimension’) inayohusika zaidi na ulimwengu wa roho na ambayo bado inaendelea kuhama mpaka dakika hii. Ndiyo maana watu wengi zaidi wanamjua Mungu kipindi hiki kuliko kipindi kingine chochote kile katika historia ya dunia yetu. Kwa sababu hiyo, Shetani hatashinda.

 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on December 08, 2017 10:10

Afrika Imekaliwa na Mizimu

[image error]



Afrika imekaliwa na mizimu. Wazungu hawataweza kumaliza mali ya Afrika. Mali ya Afrika ni ya Waafrika wenyewe. Itamalizwa na sisi wenyewe.


Afrika isomeshe watu wake, na itumie vizuri mapato yanayotokana na mauzo ya rasilimali zake kwa faida ya jumla ya wananchi wa nchi zake, kusudi baadaye wawe wataalamu wa rasilimali za nchi zao wenyewe, kuepukana na utumwa wa rasilimali. Rasilimali za Afrika zina miiko na masharti yake.



 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on December 08, 2017 09:55

December 3, 2017

Onyo

[image error]



254. Hebu hili na liwe onyo! Wakati wa kurudi kwa Bwana na Mwokozi wetu umekaribia sana, na hatuwezi kulipa gharama za kushindwa kufungua mlango! Lazima tuachane na maisha ya anasa ya dunia hii haraka iwezekanavyo, na tujifunge kibwebwe kumtafuta Bwana akiwa bado anapatikana.


Yesu anahangaika kufungua mlango wa moyo wako ili aingie, lakini mlango huo unapaswa kufunguliwa kutoka ndani. Fungua mlango wa moyo wako. Akikata tamaa atakwenda zake, na hutamsikia tena.



 •  0 comments  •  flag
Share on Twitter
Published on December 03, 2017 15:00

Kolonia Santita (Laana Ya Panthera Tigrisi)

Enock Maregesi
Riwaya ya Kiswahili ya kijasusi kutoka kwa Enock Maregesi.
Follow Enock Maregesi's blog with rss.